CHELSEA WAMUITA GUUS HIDDINK

Chelsea inafanya mazungumzo ya kumpa mkataba kocha Guus Hiddink.

Kocha huyo Mdachi tayari yupo nchini Uingereza na maafisa wa Chelsea wakifanya mazungumzo kwenye hoteli ya London.

Jana Chelse ilimtimua Mreno Jose Mourinho kufuatia matokeo mabaya ambapo kwa sasa Chelsea ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi ya Uingereza.

Mnamo mwaka 2009 Hiddink aliiongoza Chelsea kwa muda mfupi na kuipa taji la FA.

Katika kipindi hicho Hiddink aliiunganisha vema timu kwa sababu alipendwa na wachezaji wa Chelsea.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment