MREMBO KAMAZIMA KUSHINDA MISS WORLD?

Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2014, Lilian Kamazima leo Jumamosi atachuana na wenzake kuwania taji la dunia katika fainali zinazofanyika huko nchini China.

Fainali hizo zitamalizika leo kwenye mji wa Sanya nchini humo.

Kamazima alitwaa taji hilo ikiwa ni ushindi wa mezani baada ya Sitti Mtemvu kuamua kujivua ushindi.

Mwishoni mwa mwaka jana Sitti aliandamwa na skendo ya kudanganya umri ili akidhi vigezo vya kushindana kwenye mashindano hayo.

Baada ya vyombo vya habari kumsakama sana, Sitti alilazimika kuandika barua ya kujivua taji kwa aliyekuwa mratibu wa shindano la Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment