![]() |
| Ferguson |
Kocha wa zamani wa Manchester United
Sir Alex Ferguson amesema endapo mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich atamtimua
Jose Moutinho, atakuwa amefanya maamuzi ya kipuuzi na kuonyesha mfano wa
uongozi mbovu.
Ferguson ambaye enzi zake aliipatia
mataji mengi Man United, amemuelezea Mourinho kuwa ni miongoni mwa makocha bora
wa wakati wote na kumtaka atatue matatizo yanayoikumba kampeni ya Chelsea ya
kutetea taji la Ligi Kuu.
Amesema tayari tajiri huo ametimua
makocha wengi katika miaka 10 iliyopita, jambo ambalo anaamini Abramovich
atakuwa amejifunza kwa sasa.
Amesema Mourinho ameshinda taji la
Ulaya mara mbili na pia ametwaa mataji ya Ligi za nchi kwenye kila nchi
aliyokwenda.




0 comments:
Post a Comment