BONDIA MSTAAFU MAYWEATHER 'ATEKETEZA PENSHENI YAKE'

Mayweather akiwa kwenye chopa yake baada ya kuwasili nchini Ufaransa


Bondia mstaafu, tajiri Floyd Mayweather ameweka picha mbalimbali kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akionyesha jinsi anavyoponda raha za maisha yake ya kustaafu.

Picha hizo zimekuwa zikionyesha ziara mbalimbali katika nchi tofauti tofauti.
Bondia huyo mstaafu hivi karibuni alikuwa nchini Uturuki na sasa yupo nchini Ufaransa.

Kwa sasa Mayweather anazunguka pande mbalimbali za dunia akiwa na chopa yake ambapo alitoka Istanbul na kwenda Ufaransa.

Akiwa Uturuki alikutana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski.
Akiwa na kiongozi wa B4L Umit Akbulut nchini Uturuki
 
Akiwa na Podolski (kushoto)
Akiwa nchini Ufaransa


Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment