Katika hali ya kushangaza timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imerejea (Jumatano Dec 2) huku wachezaji wakionekana kutovaa sare maalum kama ilivyozoeleka.
Wachezaji hao ambao waliwasili saa 8 mchana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, walionekana kuvaa nguo tofauti huku zingine zikionekana kutokidhi maadili ya mchezaji mwenye weledi kama picha zinavyoonekana hapo juu.
Mavazi waliyovaa wachezaji hao yanaonyesha kama walikuwa wamekurupuka hivi licha ya safari yao kupangwa kwa taratibu zinazotakiwa.
Kwa kawaida nidhamu ya mchezaji huanzia nje ya uwanja kisha ndani ya uwanja, jambo ambalo likizingatiwa hata matokeo huwa mazuri.
Timu hiyo ilirejea kutoka nchini Ethiopia baada ya kukwama kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Chalenji kwa kutolewa na wenyeji Ethiopia.
Kili Stars iliondoshwa mashindanoni kwa kufungwa penati 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye muda wa kawaida.
Tayari kambi ya timu hiyo imevunjwa na wachezaji watakwenda kuungana na klabu zao za Ligi Kuu.

0 comments:
Post a Comment