| Benchi la ufundi la Man City likiwa limechanganyikiwa |
Timu ya soka ya Manchester City jioni hii imekiona
cha mtema kuni baada ya kutandikwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu soka
nchini England.
Mabao yote mawili ya Stoke yamefungwa na Arnautovic
7’ na 15’
Kufuatia kupoteza mchezo huo, Man City bado ipo
kileleni kwa muda ikiwa na pointi 29 sawa na Leicester City ambayo ipo dimbani
kuvaana na Swansea.
Endapo Leicester itashinda leo hii, itapanda tena
kileleni mwa msimamo wa Ligi kwani itakuwa imefikisha pointi 32
| Arnautovic akishangilia mabao yake leo |
| Mchoro ukionyesha jinsi Arnautovic alivyoifunga Man City bao la kwanza.Namba unazoziona ni za jenzi za wachezaji wa Stoke City |
0 comments:
Post a Comment