![]() |
| Katibu Desouza |
Kamati ya muda ya Chama cha Mchezo wa Vinyoya
Tanzania (TBA) imeiomba Kamati ya Olimpiki nchini (TOC) kuurudisha upya mchezo
huo baada ya kupotea kwa miongo miwili.
Kamati hiyo iliundwa kwa amri ya Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) ikiwa ni sehemu ya kupitia vyama mbalimbali vya michezo nchini
na kuona utendaji wake.
BMT ilibaini udhaifu mkubwa ikiwamo kutofanyika
mikutano ya kitaifa na kukosekana kwa wanachama kunakochangiwa na katiba mbovu
ya chama hicho.
Novemba mwaka huu BMT iliitangaza kamati hiyo
itakayodumu kwa siku 90 ikitakiwa kuhamasisha wanachama wapya ili kufanyika
mkutano mkuu na kuandaa mashindano.
Akizungumza wakati wa kutangaza mashindano ya mchezo
huu yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 5-6 mwaka huu, Makamu
Mwenyekiti wa kamati hiyo Timothy Kahoho alisema, “Mchezo wa vinyoya
uliing’arisha Tanzania enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere, lakini kutokana na
kukosa kuungwa mkono ulijikuta ukipotea katika medani ya kimataifa miaka 20
sasa haujashiriki katika michuano ya olimpiki”.
Kahoho alisisitiza kwamba mchezo wa vinyonya
ukirudishwa na TOC utaiwakilisha Tanzania kama awali kwani kwa miaka ambayo
haujashiriki umezifanya Uganda na Kenya kupanda viwango kutokana na serikali
zao kuunga mkono juhudi zinazofanywa.
Mbali na hilo Kahoho alitangaza kuenzi mchango wa
mwasisi wa mchezo huo nchini Marehemu Rwehabura Kente aliyefariki Machi 2015
kuanzia mwaka ujao kutakuwa na mashindano
yatakayojulikana kwa jina la Kente Cup.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TBA, Toney Desouza
alisema mashindano hayo yatawaleta pamoja wachezaji akali ya 30 kutoka
Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia kwa wanaume na wanawake (singles &
doubles).
“Viwanja vitakavyotumika katika michuano hiyo mwaka
huu ni Shuskunj, Badminton Institute na Khalsa SC maeneo ya Kisutu jijini Dar
es Salaam,” alisema Desouza

0 comments:
Post a Comment