Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea jioni ya leo kwa mechi mbili ambapo kule Tanga, Coastal Union ilikuwa inacheza na African Sports zote kutoka huko.
Mchezo mwingine ulikuwa jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Karume ambapo JKT Ruvu ilikuwa inacheza na Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.
Tukianza na kule Tanga kwenye Tanga Derby iliyopigwa kwenye dimba la Mkwakwani kwa kuwakutanisha African Sports na Coastal Union ni kwamba timu zote zimetoka sare ya 1-1.
Juma Mahadhi ndiye aliyefunga bao la Coastal Union huku Mohammed Mtindi naye akiwafungia Wana Kimanumanu bao lao.
Wakati huo huo, JKT Ruvu wamewapa somo maafande wa Magereza Prisons kwa kuwachapa mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara leo.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Samwel Kamuntu alifunga bao moja, Mussa Juma akatupia moja na Michael Aidan akifunga moja huku lile la Prisons likifungwa na Mohammed Mkopi

0 comments:
Post a Comment