ARSENAL YAONGOZA LIGI

Timu ya soka ya Arsenal jioni ya leo imefanikiwa kuitungua Aston Villa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi kuu England.

Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Olivier Giroud kwa penalti dakika ya nane baada ya The Walcott kuonekana ameangushwa na lingine Aaron Ramsey dakika ya 38.

Ushindi huo wa ugenini pale Villa Park unaifanya The Gunners irejee kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 16, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 32, sawa na Leicester City wakati Manchester United sasa ni ya nne kwa pointi zake 29.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment