MESSI ALAMBA TUZO ZA LA LIGA

Lionel Messi alitajwa kuwa mchezaji bora wa La Liga msimu uliopita mbele ya Ronaldo katika tuzo hizo zilizofanyika huko Barcelona.

Baada ya kuiongoza Barca kushinda treble msimu uliopita, Luis Enrique nae akatajwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora.

Messi kwa mara nyingine tena akatajwa kuwa mshindi wa tuzo mshambuliaji bora – hii ikiwa mara ya sita kushinda tuzo za uchezaji na ushambuliaji bora wa La Liga.

Neymar ambaye nae kwa mara ya kwanza ameingia kwenye top 3 ya Ballon D’or alitajwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Amerika.

Golikipa wa Barca, Claudio Bravo akashinda tuzo ya golikipa bora, huku kiungo wa Valencia Sofiane Feghouli akishinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Afrika.

Cristiano Ronaldo naye akashinda tuzo ya mashabiki, huku Sergio Ramos akishinda tuzo ya beki bora na Tuzo ya kiungo bora ikienda kwa James Rodriguez.

PICHA ZAIDI

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment