Wakati tetesi za kuondoka Real Madrid mwishoni mwa
msimu huu zikizidi kushika hatamu kwa mchezaji Cristiano Ronaldo, klabu yake ya
Real Madrid imekasirishwa na tabia mpya aliyoianzisha nahodha huyo wa Ureno.
Inaripotiwa kwamba Real Madrid wamekasirishwa na
tabia mpya ya Ronaldo kusafiri mara kwa mara kwenda barani Afrika katika nchi
ya Morocco kukutana na rafiki yake Badri Hari.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Ronaldo amekuwa
akitumia muda wake wa kupumzika jioni kwenda Morocco kukutana na bingwa wa
kickboxer, Badr Hari jijini Rabat Morocco – mji ambao upo kaskazini mwa
Morocco.
Baada ya mazoezi kila siku jioni, Ronaldo
anaripotiwa kuchukua ndege yake binafsi yenye thamani ya €19m kupaa juu ya
bahari ya Atlantic kwenda kukutana na rafiki yake kisha kurejea jijini Madrid
kwa mazoezi siku inayofuatia.
Mabosi wa Real wanapata wasiwasi na tabia hiyo ya
Robaldo na wanahisi inachangia katika kushusha kiwango cha Ronaldo msimu huu.
Baada ya Nahodha wa Ureno kufanya ziara nyingi
kwenda Morocco mwezi uliopita, picha nyingi za Hari na Ronaldo zilipostiwa
kwenye mitandao ya kijamii.
Vyombo vingi vya habari nchini Hispania vimekuwa
vikiuponda urafiki wa Ronaldo na Hari – gazeti la El Mundo limeuelezea uhusiano
huo kama mkanganyiko na huku wakimtuhumu Mmorrocco huyo amekuwa akitishia
watu na ni mgomvi ambaye muda mwingine huwaingia watu maungoni.

0 comments:
Post a Comment