Na Arone Mpanduka
Timu ya soka ya Mgambo JKT imesema imeshakamilisha kila kitu na sasa inasubiri kupambana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu.
Mgambo kesho itakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuikaribisha Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na MPANDUKA BLOG,Kocha mkuu wa Mgambo Bakari Shime alisema timu yake ipo tayari kwa mchezo huo.
Alisema lolote linaweza kutokea kwenye mchezo huo kwa sababu kila timu imejiandaa.
"Historia haitoi matokeo, hatuwezi kusema kwamba tutaifunga Yanga eti tu kwa sababu mara zote tumekuwa tukiwafunga hapa Tanga," alisema Shime.

0 comments:
Post a Comment