Siku
moja baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea
Jose Mourinho amedai kuwa wachezaji wanamsaliti
Mourinho
amesema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues
wanaibuka kidedea lakini imeshindikana.
Amesema
moja ya vipawa vyake ni uwezo wa kusoma na kuelewa mchezo kwa haraka, lakini
kwa hilo anahisi amesalitiwa.
Amesema
wakati mwingine anahisi kama vile alijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji
wake msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika
kiwango hicho.
Msimu
uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu
huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.
The
Blues sasa wapo katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zilizo
kwenye hatari ya kushuka daraja msimu ujao.
Hata
hivyo kinachomkera sana raia huyo wa Ureno ni kichapo cha 2-1 mikononi mwa
vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City.

0 comments:
Post a Comment