MPIRA WA MAGONGO KURINDIMA WIKI HII


Na Nicolaus Kilowoko

Chama cha mchezo wa Mpira wa Magongo nchini “Tanzania Baseball and Softball Association” kinatarajiwa kufanya mashindano ya mchezo huo mapema mwezi huu kuanzia Desemba 11hadi 13 mwaka huu ambapo yatafanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Azania.


Katibu Mkuu wa chama hicho Alpherio Nchimbi amesema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha timu 9 za vijana, 7 kati ya hizo ni za vilabu vya shule ya sekondari za Iyunga kutoka katika mikoa ya Mwanza,  Mwanakwerekwe, Zanzibar, Kibasila na wenyeji Azania kutoka Dar es Salaaam.

Nchimbi amesema katika mshindano ya mwaka huu kutakuwa na wataalamu wa mchezo huo kutoka nchini Japan watakaosimamia katika sehemu ya uamuzi pamoja na masuala ya ufundi kwa kusaidiana na wataalamu wa hapa nchini.

Aidha Nchimbi amesema mashindano hayo yatatumika kuteua timu ya Taifa ya mchezo huo wa baseball ya u21 yanatotarajiwa kuafanyika Afrika Kusini February 2016.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment