U15 YAREJEA DAR KINYONGE BAADA YA TRA KUFUNGA AKAUNTI TFF

Ziara ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na kufungwa akaunti za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki iliyopita kuelekea jijini Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.
Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.
Awali ziara ya timu hiyo ya U-15 ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda, Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.
U-15 inajiandaa na michuano ya Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.

IMETOLEWA NA TFF
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment