Mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini Oscar
Pistorius amepewa dhamana akisubiri hukumu ya mauaji ya mpenzi wake Reeva
Steckhamp.
Hukumu inatarajiwa kusomwa Aprili 18 mwaka ujao.
Jaji Aubrey Ledwaba amesema hakuna hatari kwamba
Pistorius anaweza kutoroka akipewa dhamana kwani alijisalimisha mahakamani
mwenyewe hii leo.
Pistorius, mwenye umri wa miaka 28, ametakiwa kulipa
randi 10,000 ($700) kama dhamana.
Ataendelea kutumikia kifungo cha nyumbani na atakuwa
na kifaa cha kumfuatilia kielektroniki.
Anaruhusiwa kuondoka nyumbani kati ya saa moja
asubuhi hadi saa sita mchana katika eneo la nusu kipenyo la kilomita 20 kutoka
kwenye nyumba anayoishi.
Pistorius pia ametakiwa kusalimisha pasipoti yake ya
kusafiria kwa mahakama.
Oscar anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 15,
ingawa jaji huenda akampunguzia hukumu.
Bingwa huyo wa Olimpiki alirejea kortini leo baada
ya mahakama ya rufaa kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini wa kumpata na
hatia ya kuua bila kukusudia na badala yake ikaagiza ahukumiwe kwa mauaji.

0 comments:
Post a Comment