NAPE NNAUYE NDIYE WAZIRI WA MICHEZO

Na Arone Mpanduka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amemteua Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo

Magufuli amemtaja Nape kushika nafasi hiyo wakati alipokuwa akitangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam mapema leo.

Kabla ya hapo Nape alikuwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mtama.

Awali Wizara hiyo ilikuwa ikifahamika kama Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na mara ya mwisho ilikuwa chini ya Dokta Fenella Mkangara aliyesaidiwa na Juma Nkamia.

Maana yake ni kwamba kwa sasa Nkamia hayupo tena kwenye Wizara hiyo huku Dokta Fenella akiwa ameshindwa kutetea ubunge katika uchaguzi uliopita.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment