Mabingwa wa Afrika, TP Mazembe sasa wamejua mpinzani
wao wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu.
Mazembe inakutana na Sanfrecce Hiroshima ya Japan
ambayo leo imeanza michuano hiyo vizuri kwa kuichapa Auckland City ya New
Zealand.
Mabao mawili ya Minagawa na Shotani, yalitosha kuwapa
ushindi wenyeji hao na sasa wanakutana na TP Mazembe Jumapili.
Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanatarajia kuongoza mashabulizi ya Mazembe ambayo tayari ipo mjini Osaka kwa
ajili ya mechi ya Jumapili.

0 comments:
Post a Comment