![]() |
| Rais Mohamed Ould Abdel Aziz |
Katika hali ya kushangaza, Rais wa nchi ya Mauritania
ameingilia kati mechi ya fainali ya Super Cup na kuamuru timu zipigiane penati
ili kupata bingwa huku zikiwa zimesalia dakika 27 kabla mchezo kumalizika.
Kwa mujibu wa sheria na kanuni za mashindano husika
ya mpira wa miguu, mchezo wowote wa fainali huamriwa kuingia kwenye hatua ya
penati tano tano mara baada ya kuchezwa kwa dakika 120 bila kupata mshindi.
Mtu pekee mwenye uwezo wa kutoa maamuzi hayo ni
refarii wa mchezo.
Lakini Rais huyo Mohamed Ould Abdel Aziz hakujali
hilo na badala yake alitumia mamlaka yake kama mkuu wa nchi na kuamuru mchezo
umalizike kwa mikwaju ya penati mara moja licha ya dakika za mchezo kutofika
mwisho.
Inaelezwa kuwa Rais huyo alikerwa na jinsi mechi
hiyo ilivyopooza ambayo ilihusisha timu ya FC Tevregh Zeina dhidi ya ACS Ksar na
ndipo ilipotimu dakika ya 63 ya mchezo akaamuru zipigwe penati ili atoke
uwanjani akafanye shughuli zingine.
Wakati penati hizo zinaamriwa kupigwa timu zote
zilikuwa zimefungana bao 1-1, na hadi mikwaju ya penati inakamilika, Zeina
ilichomoza na ubingwa na kukabidhiwa kombe.

0 comments:
Post a Comment