Timu ya soka ya Napoli usiku wa Jumatatu(Nov 30) imefanikiwa kuifunga Inter Milan mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi kuu soka nchini Italia maarufu Serie A.
Gonzalo Higuain aliweka rekodi ya aina yake kwa kufunga bao la mapema zaidi mnamo sekunde ya 64 ya mchezo.
Higuain alifunga tena bao la pili mnamo dakika ya 62 huku bao la kufuta machozi la Inter likifungwa dakika ya 67 na Ljajic.
Katika mchezo huo pia Nagatomo alitolewa nje kwa kadi nyekundu na kufanya Inter ibaki na wachezaji 10 uwanjani.
Ushindi huo wa Napoli unaifanya ikae kileleni kwa muda na kuiengua Inter na ikumbukwe safari hii Napoli inasaka ubingwa ambao mara ya mwisho ilitwaa mwaka 1990, wakati ambao Diego Maradona alikuwa akichezea timu hiyo.

0 comments:
Post a Comment