![]() |
| Yanga |
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipanga Yanga
kuanza na Cercle de Joachim ya Mauritius katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania na wawakilishi
katika Ligi ya Mabingwa ambayo ni michuano mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu.
Kwa mujibu wa ratiba ya Caf, iwapo Yanga itaifunga
timu hiyo ya Mauritius, itakutana na mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland
na APR ya Rwanda
CAF pia limeipangia Azam FC kusubiri mshindi kati ya
Bidviets Witts ya Afrika Kusini dhidi ya bingwa wa Kombe la FA nchini
Shelisheli.
![]() |
| Azam FC |
Bingwa huyo wa FA wa Shelisheli anatarajia
kupatikana wikiendi hii.
Iwapo Azam itashinda mechi yake hiyo ya kwanza,
itakutana na vigogo Club Esperance de Tunis ya Tunisia


0 comments:
Post a Comment