AFYA YA PELE YAIMARIKA

Imeripotiwa kuwa hali ya afya ya Nguli wa zamani wa soka wa Brazil, pele inaendelea vyema kufuatia upasuaji mdogo wa nyonga aliofanyiwa kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana.


Pele mwenye umri wa miaka 75 na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia alifanyiwa upasuaji huo Desemba 3 mwaka jana jijini New York.

Afisa habari wake, Pepito amesema Pele alitumia muda wake wa mapumziko aliokuwa na mabinti zake na wajukuu zake huko New York na kufanyiwa upasuaji huo.

Mwaka 2012 Pele alifanyiwa upasuaji mwingine kama huo huku mwaka jana akitumia zaidi ya wiki mbili hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa kidole tumbo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment