BEKI AGGREY MORRIS KUTIMKIA AFRIKA KUSINI

BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Aggrey Morris, anatarajia kuondoka nchini leo Jumanne saa 9.15 Alasiri na kuelekea nchini Afrika Kusini kufanyiwa matibabu ya nyuzinyuzi (ligaments) zinazounganisha mifupa ya goti lake la kulia.

Morris yuko nje ya dimba kwa takribani mwezi mmoja sasa baada ya kupata majeraha hayo alipokuwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ‘Zanzibar Heroes’, iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji, iliyofanyika nchini Ethiopia.

Akizungumza na mtandao wa azamfc.co.tz, Daktari wa Azam FC, Juma Mwimbe, ambaye ataambatana na beki huyo nchini humo, alisema matibabu yote ya Morris yatafanyika katika Hospitali ya Afrisurb iliyopo jijini Cape Town, Afrika Kusini.

“Tutaondoka leo saa 9.15 alasiri na tutafika kule majira ya saa 4 usiku, kesho tutakwenda kwenye hospitali hiyo ili Morris akafanyiwe uchunguzi baada ya hapo kama vipimo vitaonyesha anatakiwa kufanyiwa upasuaji basi atafanyiwa, lakini ataanza kwanza na uchunguzi,” alisema kwa ufupi Dk. Mwimbe

Morris amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye eneo la ulinzi la Azam FC akitengeneza kombinesheni nzuri na Muivory Coast, Pascal Wawa, kukosekana kwake kumemlazimu Kocha Mkuu Stewart Hall, amtumie kinda Abdallah Kheri ‘Sebo’, ambaye ameonekana kufanya vema mpaka sasa.

Mpaka sasa mechi za Azam FC alizozikosa Morris ni zile za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, Majimaji, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, pamoja na michezo mitatu ya  Kombe la Mapinduzi waliyochuana na Mtibwa Sugar, Yanga na Mafunzo.

CHANZO: TOVUTI YA AZAM FC
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment