KALI ONGALA KUINOA MAJIMAJI FC

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Azam ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Azam, Kali Ongala amesaini mkataba mfupi wa kuinoa timu ya Majimaji ya Songea.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Majimaji FC, John Nchimbi, Kali Ongala amesaini mkataba wa miezi sita.

Kwa kipindi kifupi Majimaji ilikuwa inacheza bila kocha mkuu baada ya mzungu Mika Lonnstrom kushindwa kurejea nchini kwa wakati tangu alipoaga kwamba anakwenda kwao kwa mapumziko.

Timu hiyo ilikuwa chini ya kocha msaidizi Hassan Banyai na katika kipindi chote hicho imeshindwa kufanya vizuri.

Kali Mangonga Ongala mara ya mwisho alikuwa anaifundisha Azam FC lakini akaomba kuachia nafasi hiyo ili aende kusoma nje ya nchi na sasa amerejea na kutua Songea.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment