Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Dr. Jonas Benedict Tiboroha
ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo ya Jangwani kutokana na
fukuto kubwa lililopo kwenye uongozi wa juu wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyoandikwa kwenye ukurasa
wa facebook wa ‘Naipenda Yanga’ ambapo kwa mujibu wa ukurasa huo, Dr. Tiboroha
ametoa sababu kadhaa za kujiuzulu wadhifa wake ndani ya Yanga.
“Mimi ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
kitivo cha Elimu ya Viungo (PE), na kwa kuondoka Yanga SC maana yake napata
wasaa mzuri wa kumtumikia mwajiri wangu, UDSM,” amesema.
Pamoja na Tiboroha kutozama ndani sana juu ya
kujiuzulu kwake, lakini inaelezwa alikuwa hana maelewano na Mwenyekiti wa
Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Isaac Chanji ambaye kwa sasa ndiye mtu
anayesikilizwa na kuaminiwa zaidi na Yusufu Manji.
Tayari Jonas Tiboroha amewasilisha barua ya
kujiuzulu kwa Mwenyekiti Yusuf Manji.
NB; KWA UNDANI ZAIDI SIKILIZA KIPINDI CHA MICHEZO CHA KUTOKA VIWANJANI CHA REDIO TUMAINI 96.5 FM

0 comments:
Post a Comment