Timu ya taifa ya Tunisia imetoa sare ya kufungana
bao 1-1 na Nigeria katika mchezo wa Kundi C Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya
Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee jana
mjini Kigali, Rwanda.
Super Eagles, ambao walihitaji ushindi kwenda Robo
Fainali, walikuwa wa kwanza kupata bao kupiyia kwa Chisom Chikatara dakika ya
51, kabla ya Tunisia kupata bao lililokataliwa dakika ya 44 kwa sababu mfungaji,
Ahmed Akaichi alikuwa amezidi.
Lakini mshambuliaji huyo aliyefunga mabao mawili
dhidi ya Guinea katika mchezo wa kwanza Jumatatu, akaifungia tena Tunisia
kuisawazishia dakika ya 60.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Niger na Guinea
zimetoa sare ya 2-2 na kufanya timu za kwenda Robo Fainali zipatikate katika
mechi za mwisho.
Mabao ya Niger yamefungwa na Youssef Alio dakika ya
36 na Adamou Musaminutes dakika ya 49, wakati ya Guinea yamefungwa na Aboubacar
Sylla dakika ya 37 na Aboubakar Bangoura dakika ya 75.
Nigeria sasa ina pointi nne na itahitaji kuwafunga
Guinea wanaoshika nafasi ya pili Jumanne ili kufuzu Robo Fainali kama vinara wa
kundi.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za Kundi D,
Zimbabwe ikimenyana na Mali na Uganda na Zambia Uwanja wa Rubavu.

0 comments:
Post a Comment