Aliyekuwa katibu mkuu wa klabu ya soka ya Simba,
Suleiman Said Suleiman maarufu kama Yelstin amefariki dunia.
Taarifa zinaeleza kuwa Yelstin ambaye hadi anakumbwa
na mauti alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), alikuwa akifanya mazoezi ya kuogelea na kisha kujihisi vibaya na
kukimbizwa hoispitali.
Inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo Suleiman
alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu,na baadae ikaelezwa kuwa
amekwishafariki dunia.
Marehemu aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo katika
miaka ya 1998-2000.
Wakati huohuo Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia
kifo cha Suleiman.
Katika salamu hizo TFF imesikitishwa
na kifo cha kiongozi huyo, ambaye alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea
kupewa jina la utani la ‘Yelstin” kutokana na ufanisi wake katika kazi na
misimamo akifananishwa na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris
Yeltsin.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa
miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki,
uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako
pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
Mazishi ya marehemu Selaman Said
‘Yelstin’ yalipangwa kufanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya
Kisutu jijini Dar es salaam.

0 comments:
Post a Comment