MDAU AHOJI, "SAMATTA KUREJEA SAA NANE USIKU ATAPOKEWA NA WANGA?"

Mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anayecheza ndani ya bara hilo Mbwana Samatta anatarajiwa kutua nchini usiku wa kuamkia kesho Jumamosi.

Samatta atarejea saa 8 usiku akiwa na tuzo yake mkononi lakini wadau wengi wa soka wamelalamikia muda huo huku lawama hizo zikienda kwa Shirikisho la soka nchini TFF kwa kushindwa kumuandalia ndege itakayotua nchini kwa muda muafaka.

Malisa Godlisten ni mmoja wa wadau hao na huu ndiyo waraka wake alioandika kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.



KWANINI TFF WANATAKA KUMHUJUMU
SAMMATA??
By Malisa GJ,
Hii nchi kuna watu wanapaswa
kupewa adhabu kali iwe fundisho. Miongoni
mwao ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na safu yake
ya uongozi.

Mbwana Sammata ameleta HESHIMA KUBWA
sana Tanzania ambayo viongozi wa kisiasa
wameshindwa kutuletea kwa miaka zaidi ya 50.
Ushindi wa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Heshima aliyotupa Sammata ni
kubwa sana na tunapaswa kuheshimu mchango
wake hasa ukizingatia kwamba amefika hapo
kwa juhudi binafsi. Sio TFF wala Serikali
zilizochangia mafanikio ya Sammata. Ni yeye
mwenyewe na Mungu wake.
So ilitakiwa TFF waweke utaratibu mzuri wa
kumpokea Samatta kwa heshima. Ikiwezekana
watu wafanye maandamano ya amani kuanzia
pale Airport wanapompokea hadi mahali
watakapokutanikia. Kama tunaandamana kwa
sababu za kisiasa kwanini tusiandamane
kumpongeza mtanzania mwenzetu aliyeitangaza
vema nchi yetu kimataifa?
Tena ingepaswa tuwe na Media Campaign
maalum ya kumpongeza Samatta. Na tufanye
"hashtag" kwenye mitandao ya kijamii kama
FB, Tweeter, Instagram etc. Tujenge ushawishi
watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa ndege wa
JNIA hadi Sammata mwenyewe asikie fahari na
ajivunie kuwa Mtanzania.
Lakini cha ajabu TFF kwa kushirikiana na CAF
wameamua kumhujumu Samatta. Na serikali
imekaa kimya as if ni sawa. Rais wa TFF Jamal
Malinzi ameandika kupitia ukurasa wake wa
Tweeter kuwa Samatta atatua nchini saa 8 za
usiku kesho jumamosi. Seriously?? Saa 8
usiku?? Apokelewe na "wanga" au??
Rafiki yangu Ezekiel Kamwaga amehoji kwanini
isitafutwe ndege ya saa 4 asubuhi kesho ili
watu waweze kujitokeza kwa wingi kumpokea?
Hivi kweli hatuwezi kum-market shujaa wetu??
Kama tulishindwa kumsaidia kufika hapo
alipofika, hata kumfanyia marketing
tunashindwa? Hivi mnadhani Samatta angekua
Mkenya angepokelewa saa 8 za usiku?? TFF
kuweni serious kidogo.

Saa 8 za usiku watu wanakoroma vitandani,
wengine wako club wameshalewa "ndovu
baridi" ndio mmeona ni muda mzuri wa
kumpokea Sammata? Wanaopokelewa usiku wa
manane ni "majambazi" sio shujaa kama
Samatta.
Halafu Malinzi kwa kujishtukia anajaribu
kupunguza ukali wa maneno na kusema eti
Sammata atatua kesho "saa 8 alfajiri". Hakuna
kitu kinachoitwa "saa 8 alfajiri" kwenye
Kiswahili. Ni saa 8 usiku. Alfajiri inaanza saa
10. Sasa hiyo alfajiri ya Malinzi ya saa 8 usiku
ameitoa wapi?
Pia utetezi wa Malinzi ni wa "kitoto sana". Sio
utetezi wa kiongozi tena wa taasisi kubwa kama
TFF. Malinzi anasema saa 8 usiku ndio muda
ambao Sammata amekatiwa ticket na Shirikisho
ls Soka Afrika (CAF ) ambaao ndio waandaaji wa
tuzo hizo. Hivi kwani kila wanachofanya CAF
lazima tukubaliane nacho bila kuhoji?
Ilipaswa TFF wajiulize kwanini CAF wamemkatia
Samatta ndege ya usiku wakati ndege za
asubuhi au mchana zipo.?? Jibu ni rahisi tu
kwamba CAF wanaendeleza juhudi zao za
kuhujumu nchi za Afrika Mashariki. Hawapendi
kabisa kuona nchi zetu za Afrika Mashariki
zikifanikiwa kisoka. Ndio maana hata kwenye
michuano ya kimataifa wamekua wakitupanga
na timu ngumu kama "Ghana, Senegal,
Cameroon, Algeria, Misri, Nigeria" etc ili
tusifike mbali.
Kwahiyo hili la kumpangia Samatta kurudi saa
8 usiku sio bahati mbaya. Itz a planned and
organized matter. Lengo lao tushindwe kumpa
Sammata mapokezi mazuri na ya heshima.
Kwahiyo ilitakiwa viongozi wa TFF waione
hujuma hii na waikatae.
Sifa ya kiongozi (Leader) ni kuona pale ambapo
wengine hawawezi kuona. So TFF walitakiwa
waone kuwa muda aliopangiwa Sammata (saa 8
usiku) ni hujuma za CAF, then wafikirie mbinu
mbadala ya kukataa hujuma hiyo. Ikiwezekana
kumfanyia booking upya Samatta ili atue nchini
Asubuhi, Mchana au jioni muda ambao watu
wengi wanaweza kujitokeza kumpokea.

Ingekua Sammata ni mKenya;
wangekataa hiyo ticket ya CAF ya saa 8 usiku.
Then wangemfanyia booking upya Samatta kwa
pesa zao ili aweze kutua kwa muda wanaotaka
wao. Na ingewezekana wangemtumia hata
ndege maalumu ya kwenda kumchukua.
Lakini hapa bongo TFF wamekaa tu, wanakimbilia kuandika Tweeter bila
aibu eti Samatta atatua kesho saa 8 usiku.

Natoa wito kwa watumiaji wote wa mitandao
Tushikamane kwa umoja wetu bila kujali vyama
vyetu, dini, kabila au timu tunazoshabikia,
tupige kelele mitandaoni kuhakikisha Samatta
anatua nchini muda ambao watanzania
tunaweza kwenda kumpokea.
Kama itakosekana ndege ya kesho mchana bora
aje Jumapili asubuhi kuliko kuja hiyo kesho saa
8 usiku. Share ujumbe huu, mtag kiongozi
yeyote wa Serikali au wa TFF. Kama una namba
zao wapigie au watumie sms kuonesha kulaani
hujuma inayotaka kufanywa dhidi ya Sammata
ya kumpokea saa 8 za usiku.
Tunamtaka Sammata muda ambao tunaweza
kumpokea sio saa 8 za usiku.
# JUSTICE_4_SAMMATA .!
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment