MESSI ALAMBA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA USIKU HUU

Lionel Messi ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mara ya tano.

Messi amenyakua Ballon d’Or ya FIFA akiwabwaga wapinzani wake, Mbrazil Neymar anayecheza naye Barca na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid katika hafla inayoendelea usiku huu mjini Zurich, Uswisi.

Lionel Messi amepata asilimia 41.33 ya kura zote akifuatiwa na Cristiano Ronaldo wa Ureno aliyepata asilimia 27.76, wakati Neymar anayeingia fainali kwa mara ya kwanza, amepata asilimia 7.86.

Mafanikio hayo yanakuja baada ya Messi kucheza mechi 53 mwaka jana akiwa na Barcelona, kufunga mabao 48 na kusababisha mabao 23, ingawa Cristiano Ronaldo alifanya vizuri zaidi, akifunga mabao 54 katika mechi 52 za Real Madrid.

WASHINDI KWA UJUMLA

Ballon d'or: Lionel Messi

Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka; Carli Lloyd

Tuzo ya Puskas: Wendell Lira

Kocha Bora wa Kiume wa Mwaka; Luis Enrique

Kocha Bora wa Kike wa Mwaka; Jill Ellis 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment