Rafael Nadal ameondolewa kwenye raundi ya kwanza
katika mashindano ya tenisi ya Australian Open baada ya kufungwa kwa seti tano
na Fernando Verdasco.
Hii ni mara ya kwanza kwa Nadal kuondolewa kwenye
shindano katika raundi ya kwanza.
Wachezaji hao wawili kutoka Uhispania, wanaotumia
mikono ya kushoto, walikabiliana katika uwanja wa Rod Laver Arena kwa zaidi ya
saa nne na dakika 40.
Verdasco alishinda 7-6 (8-6) 4-6 3-6 7-6 (4-7) 6-2.
Mwanatenisi huyo aliyeorodheshwa nambari 45 duniani
sasa atakutana na Dudi Sela kutoka Israel raundi ya pili.
“Nilicheza vyema sana raundi ya tano. Sijui
nilifanikiwa vipi. Nilifunga macho yangu na kila kitu kikawa sawa,” amesema
Verdasco, 32.
Verdasco alishindwa na Nadal nusufainali za 2009.

0 comments:
Post a Comment