SAMATTA AZAWADIWA KIWANJA NA SERIKALI, PIA KUJENGEWA MNARA WA KUMBUKUMBU

Selikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imemkabidhi mshambuliaji Mbwana Samatta kiwanja eneo la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kujali na kuthamini heshima ambayo nyota huyo ameiletea Tanzania ya kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (ligi za Afrika).

Samatta amepewa kiwanja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi kwenye sherehe maalum ya kumpongeza Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo hiyo iliyoipa heshima kubwa Tanzania. Tuzo hizo zimefanyika usiku wa Jumanne January 12, 2016.

Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Serikali pia imetoa pesa tasilimu kwa Samatta ambazo hata hivyo kiasi hakikuwekwa wazi.

Serikali pia imeliagiza Shirikisho la soka nchini TFF kuuboresha uwanja aliokuwa anautumia Samatta huko Mbagala kwa kuutengeneza vizuri na kujenga mnara wa kumbukumbu ya mchezaji huyo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment