Timu ya soka ya Mtibwa Sugar usiku wa leo itashuka dimbani
kuwania Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Mtibwa Sugar imeingia Fainali baada ya kuwatoa
waliokuwa mabingwa watetezi, Simba SC Jumapili kwa kuwafunga bao 1-0.
URA nayo imetinga fainali, baada ya kuwatoa mabingwa
wa Tanzania Bara, Yanga SC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika
90.
Hii itakuwa mara ya tano kwa Mtibwa Sugar kufika
fainali, baada ya awali kucheza fainali nne na kutwaa taji mara moja, 2010
ilipoifunga Ocean View ya Zanzibar.
Mtibwa iliingia fainali mwaka 2007 na kufungwa na
Yanga SC – wakati 2008 na 2015 ilifungwa na Simba SC mara zote.
URA ambao wanacheza mashindano haya kwa mara ya
pili, hawajawahi kufika fainali, lakini mwaka 2014 taji la Mapinduzi lilipanda
ndege kwenda Uganda, lilipochukuliwa na KCCA walioifunga Simba SC katika
fainali.

0 comments:
Post a Comment