SIMBA YAMIMINWA ZENJI,MTIBWA YATINGA FAINALI

Simba imeshindwa kutinga hatua ya fainali baada ya jioni ya leo kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa michuano ya Mapinduzi.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Amaan Zanzibar, Mtibwa imepata bao hilo kupitia kwa Jeba katika dakika ya 45.

Mtibwa ilionekana kucheza vizuri lakini haikuwa makini katika kumalizia kwani ilifika mara kadhaa kwenye eneo la hatari la Simba.

Katika dakika za mwisho za mchezo kipa wa Mtibwa Said Mohamed alionekana kupoteza muda kwa kujiangusha mara kwa mara.

Nusu fainali nyingine ni saa 2:15 usiku wa leo kati ya Yanga na URA ya Uganda.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment