Yanga imeshindwa kusonga mbele kwenda fainali ya michuano ya mapinduzi baada ya usiku huu kukubali kichapo kutoka kwa URA ya Uganda.
Katika mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulioanza saa 2:15 usiku, hadi dakika 90 zinakwisha timu zote zilitoka sare ya 1-1.
Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Amis Tambwe dakika ya 13 na mnamo dakika ya 77 Lwasa aliisawazishia URA.
Baada ya sare hiyo ndipo ilimlazimu mwamuzi kutenga penati tano tano ili kumpata mshindi na ndipo URA ikashinda kwa penati 4-3.
Kwa kichapo hicho Yanga ataungana na Simba kupanda boti moja kurejea Dar es salaam kufuatia Simba kufungwa mapema leo bao 1-0 na Mtibwa.
Fainali ya mashindano hayo ni Jumatano ambapo Mtibwa itakumbana na URA.

0 comments:
Post a Comment