URA ya Uganda imefanikiwa kutwaa taji la Mapinduzi usiku huu wa Januari 13 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan huko Zanzibar.
Mabao ya URA yamefungwa na Ntambi katika dakika ya 16 na Lwasa katika dakika za 86 na 88 huku la Mtibwa likifungwa na Juma Salum dakika ya 92.
Kwa ushindi huo URA imekabidhiwa kombe na kiasi cha shilingi milioni 10 huku Mtibwa ikiambulia milioni tano.
Katika hali ya kushangaza fedha zote hizo wamekabidhiwa mkononi.
Mtibwa Sugar iliingia Fainali baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Simba SC Jumapili kwa kuwafunga bao 1-0.
URA nayo ilitinga fainali, baada ya kuwatoa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Hii ni mara ya tano kwa Mtibwa Sugar kucheza fainali, baada ya awali kucheza fainali nne na kutwaa taji mara moja, 2010 ilipoifunga Ocean View ya Zanzibar.
Mtibwa iliingia fainali mwaka 2007 na kufungwa na Yanga SC – wakati 2008 na 2015 ilifungwa na Simba SC mara zote na mwaka huu imeingia lakini imeendelea kutoka kapa.

0 comments:
Post a Comment