BAADA YA SAFARI KUPIGWA DANADANA, YANGA YAPAA

Baada ya safari yake kupigwa danadana kadhaa, hatimaye timu ya Yanga imepaa jioni hii kwenda Mauritius kwa ajili ya kucheza mechi yake ya kwanza ya mashindano ya Klabu bingwa Afrika dhidi ya Cecle de Joachim.

Yanga ambayo ilitua kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo, walijikuta wakikaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa 12 wakisubiri matengenezo ya ndege ya moja kwa moja waliyoikodi.

Mechi hiyo itapigwa kesho Jumamosi saa 9 alasiri kwa saa za Mauritius.

Yanga ilikuwa ipae tangu Jumatano iliyopita lakini safari iliahirishwa kwa lengo la kuepuka kuchosha wachezaji kwa ndege za kuunganisha.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment