'TFF' YA KENYA YAPATA RAIS

Mwenyekiti wa klabu inayocheza ligi ya daraja la chini nchini Kenya Nicholas Mwendwa ameteuliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka Kenya (FKF).

Bw Mwendwa amechaguliwa kwenye uchaguzi wa taifa wa shirikisho hilo ambao ulifanyika Kasarani, Nairobi.

Aliungwa mkono na wajumbe 50 kati ya wajumbe wote 77 na kuwashinda Bw Ambrose Rachier na Ssemi Aina.

Aliyekuwa rais kwa miaka minne, Bw Sam Nyamweya, alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi muda mfupi kabla ya kura kupigwa.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment