Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi
alikosa mazoezi siku ya Jumatatu ili kupimwa figo yake.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikosa
kucheza mechi ya nusu fainali ya klabu bingwa duniani baada ya kupatikana na
tatizo la figo,baada ya kuwa na maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mawe ndani
ya figo.
Hatahivyo alifanikiwa kushiriki katika fainali ya
michuano hiyo siku tatu baadaye na ameichezea timu yake katika mechi zake zote
za ligi.
Taarifa ya klabu ya Barcelona imesema kuwa Messi
mwenye umri wa miaka 28 atarudi katika hali yake ya kawaida siku ya Jumatano.
Messi amefunga mabao 12 katika mechi 17 za ligi ya
La Liga msimu huu na kuisaidia Barcelona kupanda pointi tatu juu ya jedwali la
ligi hiyo.

0 comments:
Post a Comment