Na Arone Mpanduka
Kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya soka ya Yanga
kesho kitapaa kwenda nchini Mauritius kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Klabu
Bingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao
makuu ya Klabu hiyo yaliyoko mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam,
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Murro amesema
Yanga itasafiri na watu saba wa benchi la ufundi na baadhi ya viongozi huku
mkuu wa msafara akitarajiwa kuwa Ayoub Nyenzi kutoka Shirikisho la soka nchini
TFF.
Amesema kwa mujibu wa taarifa walizopata kutoka Mauritius
ni kwamba mchezo wao utachezwa Februari 13 mwaka huu.
Wakati hayo yakiendelea, Shirikisho la soka nchini
TFF limezitakia kila lakheri timu zinazowakilisha nchi katika mashindano ya
kimataifa ngazi ya vilabu.
Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine amesema jambo
kubwa ambalo timu zinapaswa kufanya ni kuwa na nidhamu ili zifanikiwe katika
michuano hiyo.

0 comments:
Post a Comment