Kocha mpya wa timu ya Newcastle United Rafa Benitez leo ameanza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo.
Benitez ambaye aliwasili Tyneside saa chache kabla ya Steve McClaren kutimuliwa kazi Ijumaa ya jana, ameingia kandarasi ya miaka mitatu.
Habari za uhakika zinasema kwamba Benitez ambaye alilkuwa hana kazi tangu alipotimuliwa na Real Madrid mwezi Januari atasitishiwa mkataba wake kama timu hiyo itashuka daraja.
Bosi huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea amepewa nafasi ya kuamua kuunda upya benchi lake la ufundi.
McClaren amefutwa kazi na Newcastle ikiwa ni baada ya miezi tisa ambapo ameshinda michezo sita kati ya michezo 28 na anaiacha timu hiyo katika nafasi ya 19 katika masimamo wa ligi alama moja zaidi ya nafasi salama.
Benitez anakuwa meneja wa 8 kudumu katika kipindi cha miaka 12 iliyopita huku akiwa ni meneja wa pili wa kigeni katika ‘Premier League’ akimfuatia Ruud Gullit.
Mhispania huyo ameshinda mataji 12 yakiwemo mawili ya ‘La Liga’ alipokuwa na Valencia na lingine kubwa la ‘Champions League’ alipokuwa na Liverpool katika kipindi chake cha mafanikio.

0 comments:
Post a Comment