Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Arsenal Arsene Wenger
amethibitisha kuwa mchezaji wake Alex Oxlade-Chamberlain atakaa nje ya uwanja
kwa muda wa wiki 6 hadi 8 lakini haitaji upasuaji katika mguu wake.
Kiungo huyo wa pembeni alipata majeraha hayo ya mguu
katika uwanja wa Emirates baada ya kugongana na mchezaji wa Barcelona Javier
Mascherano katika mchezo wa mabingwa barani Ulaya.
Oxlade-Chamberlain anaweza akikosa michezo ambayo
kalabu yake itakuwa ikicheza na anaweza akawaamepona wakati kocha mkuu wa timu
ya Taifa ya uingereza Roy Hodgson's atakapo
chagua wachezaji katika michuano ya Euro 2016.
Wenger amesema baada ya klabu yake kupata ushindi
katika mchezo a ngao ya jamii dhidi ya Chelsea,mchezaji huyo mwenye miaka 22
alikuwa anahangaika kurudi katika katika kiwango chake.

0 comments:
Post a Comment