Rais mpya wa Fifa, Gianni Infantino ametoa kali ya
mwaka siku alipoingia ofisini baada ya kuamua apokelewe kwa kucheza mechi.
Wakati wengine wakitarajia aingie na kuanza kazi
ofisini, yeye aliwaalika nyota wa zamani wa soka, halafu ikachezwa mechi.
Mechi ya kumpokea ilikuwa ni kati ya maofisa wa FIFA
dhidi ya nyota hao, mechi iliyopigwa mwenye moja ya viwanja vilivyo katika
ofisi za Fifa.
Infantino mwenye miaka 45, aliwaalika nyota waliotamba
zamani kama Deco, Luis Figo, Michel Salgado, Fabio Cannavaro, Paolo Maldini,
Clarence Seedorf na wengine kwa ajili ya mechi hiyo ya burudani.
Infantino ameshinda urais wa Fifa kwa kupata kura
112 akichukua nafasi ya Sepp Blatter baada ya kumshinda rais wa Shirikisho la
Soka la Bahrain, Sheik Salman bin Ebrahim Al Khalifa.
CHEKI JINSI ALIVYOKUWA AKISAKATA SOKA




0 comments:
Post a Comment