KUELEKEA MECHI YA YANGA NA APR, BABA MZAZI WA FRANCIS CHEKA KAYASEMA HAYA

Yanga inashuka dimbani kesho Jumamosi kuivaa APR ya Rwanda huku kibindoni ikiwa na mabao mawili ya ugenini.

Katika mchezo wa kwanza Yanga iliifunga APR nyumbani mabao 2-1.

Tayari APR wametua nchini jana kwa ajili ya mchezo huo.

Kuelekea kwenye mchezo huo,baba mzazi wa bondia Francis Cheka, mzee Boniface Cheka amesema ana wasiwasi na safu ya ulinzi ya Yanga.

Akizungumza na MPANDUKA BLOG, mzee huyo amesema mabeki wa Yanga wamekosa umakini katika mechi za hivi karibuni, jambo ambalo huenda likawagharimu katika mechi zake zijazo.

Alisema kuna wakati mabeki hao wamekuwa wakitegeana wenyewe kwa wenyewe ama kutegea mipira ya timu pinzani ili waonekane wameotea.

"Mimi ni mpenzi mkubwa wa Yanga na huwa sipendi kuona wachezaji wangu wanafanya mizaha"
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment