Simba imeendeleza wimbi la ushindi Jumamosi ya leo
kwa kuifunga Coastal Union mabao 2-0.
Mabao ya Danny Lyanga na Hamis Kiiza yameipa Simba pointi
tatu kwenye uwanja wa Mkwakwani na sasa imefikisha jumla ya pointi 57 baada ya
kucheza michezo 24 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Simba sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba
dhidi ya wapinzani wake kwenye mbio za ubingwa Yanga na Azam zenye pointi 50
kila moja huku zikiwa zimecheza mechi 21 mechi tatu nyuma ya Simba.

0 comments:
Post a Comment