MECHI YA STARS NA CHAD YAYEYUKA, CHAD YAWEKA MPIRA KWAPANI

Chad imejitoa kwenye michuano ya kuwania kucheza Kombe la Afcon.

Kwa uamuzi huo, maana yake mechi kati ya Chad na Taifa Stars iliyokuwa ichezwe kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam haitochezwa tena.

Chad imejitoa kwa madai ya kukosa fedha za safari na malazi ya timu.

Kufuatia hali hiyo Shirikisho la Soka Africa (Caf), limetangaza kuiondoa Chad katika michuano ijayo kuwania kufuzu kucheza Afcon na mingine yote iliyo chini yake.

Kama hiyo haitoshi, Caf imetangaza kuitwanga Chad faini ya dolla 20,000 (zaidi ya Sh milioni 44) kutokana na kitendo chake cha kujiondoa katika michuano ya ya kuwania kucheza Afcon.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuwa imetwangwa bao 1-0 kwao
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment