KASHFA YA RUSHWA YAPEPERUSHA MDHAMINI WA TIMU YA GEITA

Mgodi wa dhahabu wa Geita ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Geita Gold Sports umesitisha udhamini wake kwa muda kwa klabu hiyo inayotuhumiwa kupanga matokeo ya ligi daraja la kwanza.

Msemaji wa mgoni huo Tenga bin Tenga amesema licha ya Geita Gold Sports kuwaandikia barua ya kujitetea kwamba haihusiki na kashfa hiyo, mgodi kwa sasa hautahusika na udhamini wowote hadi pale ukweli halisi wa tuhuma hizo utakapobainika.

“Baada ya tu ya timu kutuhumiwa kwamba imetumia rushwa na kupanga matokeo, haraka uongozi wa mgodi wa Geita ukaiandikia timu barua kwamba iwezekutoa ufafanuzi wa jambo hili ambalo linazunguzwa”, amesema Tenga.

“Timu ilichofanya, ilijibu na kusema hawana hatia yoyote na hawajafanya kitendo kama hicho lakini kama uongozi unahakikisha sheria na taratibu zinafuatwa, mgodi ulichofanya ni kusitisha udhamini tukisubiri upelelezi na uchunguzi wa TFF pamoja na chunguzi nyingine ili ziweze kutoa majibu yanayofaa katika kufanya maamuzi”.

“ Kwahiyo kwasasa mgodi umesitisha udhamini ukitegemea kutoa maamuzi sahihi pale ambabo taratibu zote za uchunguzi zimeshapata majibu”.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment