LIVERPOOL YAANZA ROBO FAINALI KWA SARE

Michezo minne ya robo fainali ya michuano ya Europa League usiku wa Alhamis imechezwa katika viwanja vinne tofauti.

Liverpool wakiwa ugenini nchini Ujerumani walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Borrusia Dortmund, Divock Origi aliwafungia Liverpool bao la kuongoza kabla ya beki wa Dortmund Mats Hummels kusawazisha.

Sevilla wakawachapa ndugu zao wa Athletic Bilbao kwa mabao 2-1mabao ya ushindi ya Sevilla yakifungwa na Timothee Kolodziejczak na Vicente Iborra, huku bao la kufutia machozi la Bilbao likifungwa na Aduriz Zubeldia.

Sporting Braga wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk walikubali kulala kwa kichapo cha mabao 2-1,wachezaji Yaloslav Rakitskiy na Facundo Ferreyra wakifunga mabao ya ushindi, huku Naval Costa Eduardo kwa Braga.

Villarreal wakicheza katika dimba la El Madrigal wlichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sparta Prague, Cedric Bakambu akifunga mabao yote mawili kwa upande Villareal huku Jakub Brabec akifunga bao pekee la Sparta.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment