MALINZI AZUA KIZAA ZAA MTANDAONI

Na Arone Mpanduka

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi amezua kizaa zaa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya jana kuweka msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara wenye maandishi ya kishabiki.

Malinzi aliweka msimamo huo muda mchache baada ya kumalizika kwa mechi tatu za Ligi Kuu Tanzania bara.

Kilichozua kizaa zaa ni kitendo cha picha ya msimamo huo kwa nyuma yake kuonesha maandishi yasomekayo 'Naipenda Yanga'.

Maandishi hayo hayaonekani kirahisi isipokuwa inahitaji mtu achunguze sana picha hiyo.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya miaka kumi iliyopita Malinzi aliwahi kuwa kiongozi katika klabu ya Yanga.

Picha hiyo ya msimamo ilileta zogo ambapo wadau mbalimbali walimshambulia Malinzi wakidai kwamba hakufanya kitendo cha kiungwana kwa kuanika hadharani mahaba yake kwa timu ya Yanga ambayo baada ya ushindi wa jana dhidi ya Mtibwa ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Hata hivyo kupitia majibishano hayo, Malinzi alijitetea kwa kusema kwamba msimamo huo aliu-retweet, akimaanisha aliutoa sehemu na kuamua kuuweka kwenye ukurasa wake.


Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment