Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kutamba na miondoko ya soukous, Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia.
Papa Wemba amefariki dunia leo April 24 ,2016 baada ya jana kuanguka ghafla wakati akiwa anatumbuiza jukwaani huko Abijan nchini Ivory Coast.
Nguli huyo mwenye uraia wa Congo ambaye alizaliwa mwaka 1949 huko Wilayani Sankuru nchini Congo DR, kwa mara ya kwanza alijiunga na kundi la miondoko ya Soukous la Zaiko Langa Langa mnamo mwaka 1969.
Katika kundi hilo alifanya kazi na wakongwe muziki kama vile Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole na wengineo.
Mnamo mwezi Februari mwaka 1977, Papa Wemba alianzisha kundi lake mwenyewe la Viva la Musica ambalo lilitoa vipaji vingi sana wakiwemo wanamuziki nguli wanaotamba duniani kwa sasa.
Wanamuziki hao walipita kwenye kundi hilo kwa nyakati tofauti tofauti kwa mfano Fafa de Molokai, Debs Debaba, King Kester Emeneya (1977–82), Koffi Olomide, as a singer, (1978–79), Djuna Djanana (1978–81), Dindo Yogo (1979–1981), Maray-Maray (1980–84), Lidjo Kwempa (1982–2001), Reddy Amissi (1982–2001), Stino Mubi (1983–2001) na wengineo.
Miongoni mwa vibao vyake vilivyowahi kutikisa ni pamoja na "L'Esclave" (1986), "Le Voyageur, Maria Valencia" (1992), "Foridoles, Dixieme Commandement" (1994), "Emotion" (1995), "Pole Position" (1996), "Bakala dia Kuba" (2001), na "Somo Trop" (2003)
Marehemu Papa Wemba pia alijaaliwa kipaji cha uigizaji ambapo mwaka 1987 aliigiza katika filamu ya Kikongomani iitwayo La Vie est Belle

0 comments:
Post a Comment