Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea kwa michezo
miwili ya robo fainali kuchezwa usiku wa jana(Jumatano April 6).
Wolfsburg wakiutumia vyema uwanja wao wa Volkswagen
Arena, wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid.
Ricardo Rodriguez ndiye alianza kuipatia timu yake
bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Andre Schurrle kufanyiwa madhambi
na Casemiro.
Katika dakika ya 18 Max Arnold akaongeza bao la pili
na kuwazamisha kabisa vijana wa Zidane.
Nao Man City wakicheza ugenini huko nchini Ufaransa
walikwenda sare ya kufunga kwa mabao 2-2, mabao ya Psg yalifungwa na
mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Adrien Rabiot.
Huku mabao ya Man City yakifungwa na viungo Kevin De
Bruyne na Fernandinho, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic alikosa mkwaju wa penati
uliokolewa na kipa Joe Hart.

0 comments:
Post a Comment